BONGO5 officially launched PEOPLE AWARDS OF TANZANIA

Posted on

Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5, Nancy Sumari (katikati), Mhariri wa Bongo5, Fredrick Bundala(kulia) wakizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 Media Group, Nancy Sumari, amesema tuzo za watu Tanzania ni za kwanza za aina yake na zina lengo la kuwatambua watu wanaofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali.

Naye Mhariri wa mtandao wa Bongo5, Fredrick Bundala amevitaja vipengele vitakavyowaniwa mwaka huu kuwa ni pamoja na:
1. Mtangazaji wa redio anayependwa
2. Kipindi cha redio kinachopendwa
3. Mtangazaji wa runinga anayependwa
4. Kipindi cha runinga kinachopendwa
5. Mwanamichezo anayependwa
6. Muongozaji wa video za muziki anayependwa
7.Video ya muziki inayopendwa ya mwanamuziki wa kiume
8. Video ya muziki inayopendwa ya mwanamuziki wa kike
9. Filamu inayopendwa
10.Msanii wa kike kwenye filamu anayependwa
11. Msanii wa kiume kwenye filamu anayependwa
Bundala amesema mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili. Kwanza ni kwa kutumia tovuti ya tuzo hizi ambayo itakua www.tuzozetu.com .
“Katika tovuti hii, mpigaji kura atakutana na hatua rahisi ya kupendekeza majina katika vipengele vyote 11 vya tuzo za watu Tanzania. Njia ya pili ni kupitia simu ya mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, ambapo mpiga kura atahitajika kuandika neno ‘TUZO’ kwenda namba 15678. Baada ya kutuma ujumbe huu, ataletewa vipengele vyote 11 vikiambatanishwa na TZW kifupi cha Tuzo Za Watu, pamoja na namba ya kila kipengele. Ili kutaja ama kupendekeza jina, atahitjika kutuma ‘code’ husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano TZW1 Michael Jackson,”amesema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s